Wednesday, December 12, 2007

hii toto jinga

Najua kuna watu ambao watadhani au hata kusema kwamba mimi nina fitina na Raila, au hata mwenzake Kalonzo Musyoka. Lakini, huo sio ukweli. Ndiyo, ni kweli kuwa hawa watu siwapendi; lakini sio nafsi zao. Mimi sina chuki kamwe na Raila mwenyewe kama Mkenya; ila nina ona aibu kila mara anapofungua wazi kinywa chake kusema lolote. Kwani kila mara itakuwa ni uwongo, au kujaribu kulaumu wengine kwa sababu ya shida zilizoko Kenya. Nia yake siijui; inawezakana anaitakia Kenya mema; lakini ni dhahiri kuwa hana mbinu yeyote kuilekeza nchi yetu tunakotaka kwenda. Haswa, maswala haya kuhusu Raila yananichukiza kweli

a) Raila, kama nilivyogundua, anadhaminiwa na wageni ambao hawatujali masilahi. Hawa ni Wajerumani, Wamarekani, Waingereza na wengineo. Miaka michache iliyopita, waliwaua ndugu zetu nakuwashtumu na kuwabatiza magaidi(unakumbuka MauMau?)

b) Kiongozi tunayestahili Kenya ni kiongozi ambaye anaelewa maana ya kuwa huru; kwahivyo, fikira na maoni yake yafaa kuwa ya asili ya Kikenya. Ni dhahiri kwamba hana ujuzi wa kuboresha uchumi.

c) Raila ni mtu ambaye ujuzi wake na pengine kipawa chake ni kusambaratisha umoja na undugu. Kwanini nasema hivyo? Waulize wakenya kadhaa, na usiulize watu wa kabila moja, ni nani ambaye wanaamini kuwa nguvu zake zinatokea katika swala la ukabila. Raila, anapoona siasa zake hazina waskilizaji, huanza kukumbusha Waluo wenzake, ambayo pengina hawaelewi mambo yalivyo au pengine wenyewe wana nia zao, kuwa Wakikuyu ni adui. Naamini Waluo ni watu ambao wanauwezo wa kuwa katika nafasi ya mbele kwa kuleta maendeleo Kenya, wakiwa na viongozi ambao hawana ubinafsi, na ambao wanaweza kusema jinsi watakavyo weza kufanya mabadiliko nchini bila kuelekeza vidole kwa wengine wakiwalaumu.Sababu zingine zi njiani!